• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Alexis Sanchez aingárisha Arsenal dhidi ya Sunderland

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:39:44

    Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez, ameisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa magoli 2 kwa 0 dhidi ya Sunderland, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Emirates na hivyo kuiwezesha klabu hiyo kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya. Sasa Gunners inahitaji kuwashinda watoto wa David Moyes, ili waweze kufanikiwa kumaliza katika nafasi nne za juu za ligi kuu nchini Uingereza.

    Katika mchezo huo ulioonekana kuwa mgumu, Sanchez aliwezesha klabu yake kuchomoza na ushindi huo. Arsenal iliyopo katika moto mkali chini ya kocha wake, Arsene Wenger, hiakuwahi kumaliza nje ya nne bora katika misimu yote.

    Kwa ushindi wa Manchester City dhidi ya West Brom unatoa tafsiri ya klabu ya Arsenal kuhitaji ushindi wa lazima katika mchezo wao wa jumapili dhidid ya Everton huku ikiombea mabaya Liverpool katika mchezo wao dhidi ya Middlesbrough.

    Bado kuna siri kubwa kama Mzee Wenger ataendelea kusalia katika nafasi hiyo ya ukocha, fumbo hili litafumbuliwa mpaka itakapo tangazwa kama atasaini Mkataba mpya ndani ya Arsenal, mpaka sasa mashabiki wa klabu hiyo hawataki kuona Mzee huyo akiendelea kusalia ndani ya klabu ya The Gurners.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako