• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sharapova anyimwa kadi ya kuingia kwenye mashindano ya French Open

  (GMT+08:00) 2017-05-18 09:43:27

  Nyota wa tenisi kutoka Urusi Maria Sharapova, amenyimwa kadi maalumu ya kuingia kwenye mashindano ya French Open yatakayoanza baadae mwezi huu.

  Mkuu wa chama cha tenisi nchini Ufaransa Giudicelli Ferrandini amesema mwaliko huo ungeliweza kutolewa kwa mchezaji ambaye awali alikuwa majeruhi lakini sio kwa aliyefungiwa kwa kashfa ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.

  Sharapova, mshindi mara tano wa Grand Slam, alimaliza kifungo cha miezi 15 hivi karibuni na hakuwa na alama za kutosha za kuingia katika droo kubwa ya kushiriki michuano hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako