• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtu mmoja auawa katika mlipuko wa bomu kaunti ya Mandera, Kenya

  (GMT+08:00) 2017-05-18 09:47:10
  Polisi nchini Kenya wamesema mtu mmoja aliuawa na mwengine alijeruhiwa alasiri ya jana baada ya gari waliokuwa wakisafiria kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara katika kaunti ya Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

  Polisi wamesema muhanga ni ofisa wa serikali ya Kenya na dereva wake alijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo.

  Tukio hilo limetokea siku moja baada ya shambulizi lingine la mabomu lililotokea katika kaunti ya Garissa na kusababisha vifo vya watu wanne.

  Polisi wa Kenya wameimarisha hatua za kiusalama kwenye maeneo hayo.

  Habari nyingine zimesema siku hiyo hiyo, watu wanne wakiwemo mshambuliaji wa kujitoa mhanga waliuawa katika shambulizi la mabomu katika kituo kimoja cha ukaguzi eneo la Wadajir mjini Mogadishu, na Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako