• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika kuratibu vigezo vya chakula ili kustawisha biashara ya kilimo

  (GMT+08:00) 2017-05-18 09:56:13

  Umoja wa Afrika umepanga kuratibu vigezo vya chakula kwa nchi wanachama wa wa umoja huo. Mkurugenzi wa kiufundi wa Shirika la Vigezo la Umoja wa Afrika ARSO Bw. Reuben Gisore amesema, zoezi hilo litaanza kwa kuweka vigezo vya vyakula kama vile mahindi, viazi, michele na mihogo.

  Bw. Gisore amesema lengo la kuweka vigezo vya pamoja vya chakula ni kuondoa vikwazo vya biashara vinavyowakabili wafanyabiashara wanaouza chakula kwa kuvuka mipaka.

  Mradi huo wa kuratibu vigezo vya chakula utafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, na kamati ya kiuchumi wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika. ARSO inatarajia kumaliza mchakato wa kuweka vigezo vya pamoja mwaka kesho kabla ya kuanza kushughulikia matunda na mboga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako