• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Antonio Guterres: Umoja wa Ulaya wenye nguvu na mshikamano ni muhimu kwa Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2017-05-18 09:56:40

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alipohutubia bunge la Ulaya huko Strasbourg, Ufaransa, amesisitiza kuwa mafanikio ya Umoja wa Ulaya na hatma ya Umoja wa Mataifa vimefungamana.

  Bw. Guterres amewaambia wabunge wa Ulaya kuwa Ulaya yenye nguvu na mshikamano, ni nguzo ya msingi ya Umoja wa Mataifa wenye nguvu na ufanisi.

  Katibu mkuu huyo pia ameorodhesha changamoto za kimataifa zinazohitaji juhudi za pamoja za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa, zikiwemo ongezeko la mapigano na vyanzo vinavyobadilika, ukiukaji wa haki za binadamu hasa kwa wakimbizi wanakimbia mapambano na udhaifu wa kiuchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, na madhara yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako