• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jose Mourinho akalia kuti kavu Ligi ya Uropa dhidi ya Ajax

    (GMT+08:00) 2017-05-19 08:54:13
    Ikiwa timu ya Manchester United itapoteza mchuano wake wa fainali ya Ligi ya Uropa dhidi ya Ajax Mei 24, basi Kocha wake Jose Mourinho atakuwa katika hatari ya kutimuliwa kwa kuwa atakuwa amechangia hasara ya Dola milioni 65 za Marekani.

    Mchuano huo utakaondaliwa katika Mji wa Stockholm pia utakuwa umefuta matumaini ya timu hiyo kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kufuatia kulemewa kushiriki moja kwa moja kupitia kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika nafasi nne bora.

    Ikiwa Man U watakosa kushiriki dimba hilo la Ulaya, itakuwa ni mara yake ya pili mfululizo kukosekana katika darubini hiyo ya hadhi na kupelekea adhabu ya Paundi milioni 21 kufuatia mkataba na wafadhili wao wa miaka 10 na kampuni ya Adidas. Ufadhili huo ni wa kima cha paundi 750 milioni.

    Mkurugenzi wa kifedha wa Old Trafford Cliff Baty tayari amedokeza kwa mbali kuwa haja yao kuu katika msimu huu ni kuhifadhi ufadhili wa Adidas na pia kuwa ndani ya michuano ya Klabu bora Ulaya."

    Iwapo Mourinho atapoteza mchuano huo dhidi ya Ajax, basi atakuwa ameitwika Man United hasara ya asilimia 30 katika ukadiriaji wa mapato.

    Baty amefichua kuwa dili ya ushindi katika fainali hiyo ni kuwa "mshindi atatuzwa hongera ya paundi 6.5 milioni huku atakayepoteza akipokonywa paundi milioni 3.5."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako