• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serengeti boys yazidi kungáa michuano ya AFCON

    (GMT+08:00) 2017-05-19 08:54:53
    Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 jana katika uwanja wa Stade de Amitie Libreville Gabon waliingia uwanjani kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi B wa michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 dhidi ya timu ya taifa ya Angola. Serengeti boys wamecheza mechi yao hiyo baada ya mchezo wao wa kwanza wa Kundi B kucheza dhidi ya Mali na kulazimishwa sare tasa 0-0, iliyowafanya Serengeti Boys kuingia katika mchezo dhidi ya Angola kwa nguvu zaidi ili kupata ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri, ukizingatia awali timu zote zilikuwa na point moja moja. Vijana wa Tanzania walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Angola kwenye Kundi B ambalo pia lina timu za Niger na Mali. Magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Kelvin Nashoni dakika ya 5 na kipindi cha pili dakika ya 69 Abdul Hamis Seleman akaifungia goli la ushindi Tanzania baada ya Angola kusawazisha goli la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza kupitia kwa Pedro. Kwa ushindi huo Serengeti Boys wanaongoza Kundi B. wakiwa wanasubiri matokeo ya mchezo wa Mali na Niger, Serengeti wana point nne hadi sasa na ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii wanahitaji sare dhidi ya Niger mchezo wa mwisho watakaocheza Port Gentil, Tanzania wakifuzu nusu fainali ya AFCON watakuwa wameingia moja kwa moja katika fainali za Kombe la dunia zitakazochezwa India mwishoni mwa mwaka 2017.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako