• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya viwanda Tanzania yaanza kukua

    (GMT+08:00) 2017-05-19 19:35:49

    Sekta ya viwanda nchini Tanzania imeanza kukua tangu serikali ya rais John Pombe Magufuli iingie madarakani na jumla ya miradi 393 yenye thamani ya shilingi trilioni 5.198 inayotarajiwa kuzalisha ajira 38,862 imesajiliwa nchini.

    Bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2017/18 imeongezwa katika eneo la fedha za maendeleo na kufikia shilingi bilioni 80 kutoka bilioni 40 mwaka 2016/17.

    Mbali na hayo, katika kipindi cha Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilifanikiwa kusajili jumla ya miradi 242 ya sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya viwanda 170 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 2,079 inayotarajiwa kutoa ajira mpya 17,285.

    Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji wa Tanzania Bwana Charles Mwijage amesema wizara hiyo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 122.2 kwa matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Kati ya fedha hizo matumizi ya kawaida ni shilingi bilioni 42 na matumizi ya maendeleo ni Sh bilioni 80.1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako