• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais na waziri mkuu wa Cape Verde wakutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2017-05-21 18:07:02

    Rais Jorge Carlos Fonseca wa Cape Verde na waziri mkuu Jose Ulisses Correia e Silva tarehe 20 kwa nyakati tofauti walikutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi mjini Praia.

    Rais Fonseca na Bw. Silva wamesema China ni rafiki mkubwa wa Cape Verde, na imetoa uungaji mkono na misaada mingi kwa Cape Verde. Cape Verde inapenda kuunga mkono na kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuzidisha ushirikiano kati ya pande mbili.

    Bw. Wang Yi amesema China inapenda kutekeleza maoni ya pamoja yaliyofikiwa kati ya marais wa nchi hizo mbili, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kupitia baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na baraza la China na nchi zinazotumia lugha ya Kireno. China inaikaribisha Cape Verde kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", hasa ujenzi wa njia ya hariri baharini ya karne ya 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako