• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yaharakisha kazi za kibinadamu nchini Libya

    (GMT+08:00) 2017-05-22 09:44:14

    Kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa masuala ya wakimbizi Bw. Filippo Grandi, amesema Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeharakisha kazi za kibinadamu nchini Libya ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na msukosuko wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya.

    Bw Grandi ameyasema hayo alipofanya ziara mjini Tripoli, Libya, ambako alikutana na wakimbizi katika baadhi ya vituo vya wakimbizi.

    Amesema vurugu na mchafuko nchini Libya vimetoa changamoto kubwa za kiusalama kwa mashirika ya kibinadamu likiwemo UNHCR kutoa misaada na kuwafika watu wenye mahitaji.

    Kwa mujibu wa UNHCR, watu karibu laki 3 wa Libya wamekimbia machafuko yanayoendelea nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako