• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la serikali ya Syria ladhibiti kikamilifu mji wa Homs

    (GMT+08:00) 2017-05-22 10:06:18

    Serikali ya Syria imesema kwa sasa inadhibiti kikamilifu mji wa Homs baada ya kikundi cha mwisho cha waasi kuondoka kutoka mjini humo.

    Gavana wa mkoa wa Homs ametangaza kuwa, waasi wameondoka ngome yao ya mwisho kwenye eneo la Wael, na polisi wa Syria na idara za serikali zitaingia kwenye eneo hilo kurudisha utaratibu wa kawaida.

    Kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Syria na kundi la waasi, kuanzia katikati ya mwezi Machi waasi na familia zao waliondoka kwa vikundi kutoka maeneo wanayodhibiti kaskazini mwa Syria. Habari zinasema watu 17,000 wakiwemo wapiganaji 7,000 wameshaondoka kwenye maeneo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako