• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shule ya Mwatate  Sino-Africa yatoa matumaini kwa mtoto wa kike Taita

    (GMT+08:00) 2017-05-22 10:23:36

    Kwa mwaka wa pili sasa shule ya ya Mwatate Sino-Africa iliojengwa kwa msaada wa China nchini Kenya imeendelea kupokea wanafunzi zaidi wa kike.

    Shule hii imekuwa ni ishara ya kuendeleza urafiki wa tangu jadi wa Kenya na China kwenye sekta ya elimu.

    Inapolia kengele katika Shule ya msingi ya wasichana ya Mwatate Sino-Africa ni wakati wa kurejea darasani baada ya mapumziko mafupi.

    Shule hii maalum liijengwa na serekali ya China kwa kima cha shilling millioni 128 lengo kuu ikiwa ni kutoa makao kwa watoto waliodhulumiwa kijinsia na wale waliotoka jamii maskini.

    Bibi Emily Kituri ni naibu mkuu wa shule hii.

    "Sasa tuko na wanafunzi 63 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na darasa la kwanza wako 13. Kwa kawaida wanafunzi wanaingia shuleni saa kumi na mbili na nusu asubuhi na kuna baadhi ya wanafunzi ambao wanalala shuleni. Tuliona wasichana wanapitia shida nyingi ndio maana wakaamua kujenga shule hii."

    Elimu ya watoto wa kike hapa katika kaunti ya Taita taveva inaadhiriwa na masaibu kama vile ndoa za mapema, talaka za wazazi, umaskini na tamaduni za kumpendelea mtoto wa kiume.

    Lakini sasa shule hii inatoa mwanga wa matumaini kwa mtoto wa kike.

    Shule hii imejengwa kufuatia makubaliano kati ya serikali ya China na ile ya Kenya mwaka wa 2016.

    Kupitia juhudi za serikali kuu na ile ya kaunti na pia ufadhili wa China ujenzi wa shule ulifanikiwa.

    Huyu hapa ni mke wa Gavana wa kaunti hii Hope Mruttu.

    "Wakati mume wangu alipochaguliwa kuwa Gavana wa kaunti ya Taita Taveta, nilizunguka kote kwenye kaunti hii nikitafuta ni kitu gani naweza kuwafanyia wanawake wa Taita Taveta na nikagundua kwamba sisi tuko kwenye nafasi ya nne katika matukio ya dhuluma dhidi ya wanawake na kutokana na hilo nikaanzisha kampeni kuhakikisha kwamba watoto wa kike hawadhulumiwi kingono"

    Changamoto iliopo kwa sasa ni ukosefu wa umeme kwenye shule hii lakini mazingira ya kusoma ni tulivu na wanafunzi wanafurahia kupata raslimali ilio muhimu kwa maisha yao ya baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako