• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Ethiopia laanzisha safari ya moja kwa moja kati ya Addis Ababa na Chengdu China

    (GMT+08:00) 2017-05-22 18:26:19

    Shirika la ndege la Ethiopia limeanza rasmi safari ya moja kwa moja kati ya mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia na mji wa Chengdu, China.

    Mkurugenzi mtendaji mkuu wa shirika hilo Bw. Tewolde GebreMariam amesema, China imekuwa soko kubwa zaidi kwa shirika hilo, na Chengdu ni mji wa tano nchini China kuwa na safari ya moja kwa moja kwenda Addis Ababa. .

    Balozi mdogo wa China nchini Ethiopia Bw. Liu Tao amesema Shirika la ndege la Ethiopia likiwa ni moja kati ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika, limetoa mchango mkubwa kwa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika.

    Licha ya mji wa Chengdu, shirika hilo pia lina safari za moja kwa moja kwenda miji ya Beijing, Shanghai, Guangzhou, na Hongkong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako