• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uuzaji wa vifaa vya jukwaani vilivyotengenezwa na kijiji cha Huozhuang mkoani Henan vyanufaika na maendeleo ya mtandao wa Internet

    (GMT+08:00) 2017-05-22 17:51:11

     

     

    "Shehuo" ni shughuli za burudani kwa wachina kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa Kichina, ikiwemo ngoma ya simba, na ngoma ya dragon. Utengenezaji wa vifaa vya jukwaani vya Shehuo katika kijiji cha Huozhuang mkoani Henan nchini China una historia ya miaka zaidi ya 100. Zamani wanakijiji walitengenza vifaa hivi katika karahana ndogo na mauzo ya vifaa hivi yalikabiliwa na changamoto nyingi.

    Kutokana na maendeleo na ueneaji wa mtandao wa Internet, katika miaka ya hivi karibuni kijiji cha Huozhuang kimejulikana sana na kuwa "kijiji maarufu kwenye tovuti ya Taobao", na wanakijiji wanaweza kuuza vifaa vyao nchini na nje kwa kutumia kompyuta, hali ambayo imewasaidia kuondoa umaskini na kujiendeleza.

    Mwandishi wetu wa habari aliona malori mengi ya kampuni za usafirishaji wa bidhaa yakienda na kutoka kijijini Huozhuang. Karibu kila familia ya kijiji hicho inatengeneza vifaa vya jukwaani. Mkurugenzi wa kijiji hicho Bw. Huo Junzheng alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, utengenezaji wa vifaa vya jukwaani umekuwa chanzo kikubwa cha mapato ya wanakijiji. Anasema,

    "Kijiji chetu kinatengeneza aina zaidi ya elfu moja za vifaa vya jukwaani vya Shehuo. Kazi za mikono zina historia ya miaka zaidi ya mia moja. Bidhaa zetu zinauzwa kwa Asia Kusini Mashariki, Ulaya, Marekani na sehemu mbalimbali nchini China. Kila mtu anayetumia vifaa hiyoo, anakifahamu kijiji cha Huozhuang."

    Katika miaka kadhaa ya hivi karibuni, hali mpya ya matumizi ya mtandao wa Internet ilienea nchini China. Vijana wengi waliopata elimu ya juu walianza kuwahimiza wanavijiji kutumia mtandao wa Internet, kuweka maduka kwenye tovuti ya Taobao ambayo ni mtandao mkubwa wa uuzaji nchini China. Hivi sasa wanavijiji wanaweza kuuza vifaa vyao, pia wanaweza kutafuta wateja kwa urahisi kwenye mtandao wa Internet. Mwaka jana thamani ya utengenezaji wa vifaa vya jukwaani vya Shehuo ya kijiji cha Huozhuang ilifikia yuan zaidi ya milioni 100, na kijiji hicho kilichaguliwa katika orodha ya vijiji vya Taobao mwaka 2016.

    Mwanakijiji Yao Hongyu ananufaika na mabadiliko ya njia ya uuzaji wa vifaa vya jukwaani. Amesema, tangu mwaka 2012 walipoanza kuviuza kupitia mtandao wa Internet, thamani ya biashara imeongezeka kwa mara kadhaa, na vifaa hivyo vinaweza kuuzwa kwa sehemu mbalimbali nchini humo hata nchi za nje.

    Matumizi ya mtandao wa Internet si kama tu yameshirikisha sekta ya jadi ya huko na njia ya uuzaji kwenye mtandao wa internet, pia yamekifanya kijiji cha Huozhuang kiwe mfano wa kuondoa umaskini. Mkurugenzi wa mji mdogo wa Linjin unaoongoza kijiji cha Huozhuang Bw. Huang Zhaoyu amesema, mafanikio ya kijiji cha Huozhuang yamehimiza maendeleo ya mji huo, pia yametoa njia mpya ya kuondoa umaskini. Anasema,

    "Kijiji cha Huozhuang ni kijiji cha kwanza cha Taobao mjini mwetu, kwa uongozi wa kijiji hiki, vijiji vingine jirani vinajitahidi kuiga na vimethibitishwa kuwa vijiji vya Taobao na kampuni ya Alibaba. Katika siku za baadaye, tutatumia fursa ya tovuti ya Taobao, kueneza uzoefu na kuhimiza mchakato wa kuondoa umaskini."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako