• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 71 wauawa katika operesheni mpya ya jeshi la Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-05-22 18:05:47

    Wapiganaji 71 wenye silaha wameuawa wakati wa mfululizo wa operesheni zilizofanywa na jeshi la Afghanistan siku moja iliyopita.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imesema, jeshi la ulinzi na vikosi vya usalama vya Afghanistan vilifanya operesheni 12 za kupambana na ugaidi. Wapiganaji wengine 40 walijeruhiwa katika operesheni hiyo iliyofanyika kwenye mikoa kadhaa ikiwemo Nangarhar, Helmand, Kunduz, Wardak na Zabul.

    Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza uwezekano wa vifo au majeruhi kwa vikosi vya usalama katika operesheni hiyo.

    Makundi ya Taliban na IS yanayopambana na serikali ya Afghanistan hayajatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako