• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika watoa mafunzo kwa idara za usalama nchini Somalia kuzuia matumizi ya askari watoto

    (GMT+08:00) 2017-05-23 09:28:47

    Ujumbe wa kamati ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM umemaliza mafunzo ya siku 10 kwa wawakilishi wa idara za usalama ili kuzuia matumizi ya askari watoto.

    Mafunzo hayo yameandaliwa na kitengo cha ulinzi, haki za binadamu na jinsia, na yanaendana na mpango wa AMISOM kujenga uwezo wa serikali ya Somalia.

    Taarifa iliyotolewa na AMISOM imesema waliopokea mafunzo hayo ni pamoja na washiriki kutoka serikali za mikoa na serikali kuu, na wamepewa ujuzi wa kuchukua hatua kabla ya kutuma askari, wakati operesheni zinaendelea na kuendeleza taaluma.

    Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha mafunzo ya amani na usalama cha Kenya Brigedia Patrick Nderitu, amewataka wapiganaji wote waache kutumia askari watoto, kwani utumikishaji wa watoto kwenye mapigano yanaathiri ukuaji wao wa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako