• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atuma salamu za rambirambi kwa Malkia wa Uingereza kufuatia mlipuko uliotokea Manchester

    (GMT+08:00) 2017-05-23 16:36:15

    Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kwa Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza kufuatia mlipuko uliotokea kwenye mji wa Manchester nchini humo.

    Katika salamu hizo, rais Xi ameeleza kuhuzinishwa sana na vifo vya watu wasio na hatia, na kutoa pole kwa majeruhi na familia za watu waliouawa katika tukio hilo. Amesema watu wa China wanasimama pamoja na watu wa Uingereza katika wakati huu mgumu wanaoupitia.

    Watu 22 wameuawa na wengine 59 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea nje ya Uwanja wa Manchester mara baada ya kumalizika kwa onyesho moja jana usiku.

    Naye waziri mkuu wa China Li Keqiang amemtumia salamu za rambirambi mwenzake wa Uingereza Bi. Theresa May kufuatia vifo na majeruhi yaliyotokana na mlipuko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako