• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hafla ya kuzindua ujenzi wa majengo mapya ya bunge la Jamhuri ya Congo kwa msaada wa China yafanyika

    (GMT+08:00) 2017-05-23 19:07:41

    Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo na ujumbe wa wizara ya biashara ya China wamehudhuria hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa majengo mapya ya bunge la Jamhuri ya Congo yanayojengwa kwa msaada wa China iliyofanyika jana mjini Brazaville.

    Waziri wa ardhi na miradi mikubwa wa Congo Bw. Jean Jacques Bouya amesema, nchi yake na China zinaheshimiana, kunufaishana, na uhusiano kati ya pande hizo mbili umepata na unaendelea kupata mafanikio.

    Balozi wa China nchini humo Bw. Xia Huang amesema katika miaka ya hivi karibuni nchi hizo mbili zimepata mafanikio mengi kwenye ushirikiano wa ujenzi wa miundo mbinu, safari za anga na uzalishaji. Amesema mradi wa jengo jipya la bunge utakuwa mnara mpya wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Mradi huo unaotazamiwa kumalizika mwaka 2020 ni pamoja na ujenzi wa majengo mawili yenye ghorofa tatu na ukubwa wa mita elfu 24 za mraba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako