• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yainua kiwanga cha tahadhari ya usalama hadi ngazi ya juu

    (GMT+08:00) 2017-05-24 09:21:50

    Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May ametangaza kuwa hali ya tahadhari ya kutokea kwa shambulizi la kigaidi imeinuliwa na kuwa ya juu kabisa.

    Bibi May amesema wana usalama wakiwa na silaha wamesambazwa katika nchi nzima chini ya amri ya polisi, na wataonekana katika matukio makubwa kama mechi za soka na matamasha. Bibi May amesema hayo baada ya kuendesha mkutano wa ngazi ya juu wa wana usalama, unaoitwa COBRA.

    Habari pia zinasema mtu anayetiliwa shaka amekamatwa akiwa na silaha mjini Birmingham baada ya rabsha karibu na tukio la maombolezo. Mtu huyo alikamatwa akiwa na mkoba wenye shoka na fimbo kubwa, lakini baadaye aliachiwa huru baada ya kufahamika ana matatizo ya akili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako