• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wakutana nchini Rwanda kujadili utaratibu wa watu kusafiri kwa uhuru barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-24 09:27:25

    Wataalamu kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanakutana kwa siku nne huko Kigali Rwanda kujadili rasimu ya utaratibu wa watu kusafiri kwa uhuru katika bara la Afrika.

    Mkutano huo pia unahudhuriwa na maofisa waandamizi wa serikali kutoka nchi wanachama, ambao wana kazi ya kuangalia na kutoa mapendekezo juu ya rasimu hiyo na mwongozo wake wa utekelezaji. Rasimu hiyo itajadiliwa na kupitishwa na wakuu wa nchi na serikali wakati wa Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Afrika utakaofanyika Januari mwakani.

    Akizungumzia rasimu hiyo mwenyekiti wa kamati ya utaratibu wa watu kusafiri kwa uhuru ya Umoja wa Afrika, Katyen Jackden amesema manufaa ya kuruhusu watu kusafiri kwa uhuru katika bara la Afrika yamepita changamoto za kiusalama na kiuchumi ambazo zinaweza kutokea, na kutaka kuwepo mbinu za kudumu kwa vile kila nchi ipo kwenye hatua yake ya utayari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako