• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za BRICS zaahidi kuimarisha ushirikiano katika mambo ya afya

    (GMT+08:00) 2017-05-24 18:30:56

    Mawaziri wa afya wa China, Brazil, Russia, India na Afrika Kusini nchi zinazounda kundi la BRICS walikutana jana na kubadilishana maoni kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao katika mambo ya afya, na kuahidi kuimarisha ushirikiano huo ili kuboresha afya za wananchi wa nchi hizo.

    Mawaziri hao ambao wamekutana kando ya mkutano wa 70 wa afya duniani unaofanyika Geneva, Uswisi, wamejadili masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha watu wengi zaidi kupata na kuweza kununua dawa na vifaa vya matibabu, kusukuma mbele mkakati mpya wa kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu duniani, na kuimarisha uratibu kati ya idara mbalimbali kwenye kuzuia hali ya usugu dhidi ya dawa.

    Pia wamesisitiza kuwa idadi ya watu katika nchi za BRICS inachukua zaidi ya asilimia 40 ya idadi ya watu wote duniani, hivyo sera za afya za nchi hizo ni muhimu kwa udhibiti wa maradhi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako