• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gabriel wa Arsenal nje kwa wiki nane

    (GMT+08:00) 2017-05-25 09:31:35

    Beki wa Arsenal Gabriel hatoshiriki katika fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley baada ya kupata jeraha litakalomweka nje kwa wiki nane.

    Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyebebwa katika machela na kutolewa uwanjani katika mechi ya ushindi dhidi ya Everton, siku ya Jumapili anauguza jeraha la goti.

    Beki mwenzake Laurent Koscielny pia naye hatoshiriki mechi hiyo ya fainali baada shirikisho la soka nchini Uingereza FA kukataa rufaa ya kadi nyekundi dhidi ya Everton.

    Beki mwengine wa tatu wa Arsenal Shkodran Mustafi haijulikani iwapo atacheza au la.

    Mustafi anasumbuliwa na tatizo la mshtuko baada ya kupigwa kichwani wakati wa mechi dhidi ya Sunderland. Katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatano, mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alithibitisha kwamba Gabriel hatocheza hadi mwezi Agosti.

    Aliongezea kuwa anasubiri maafisa wa matibabu kubaini hatma ya Mustafi iwapo anaweza kucheza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako