• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Uingereza wauthibitisha mlipuko wa Manchester kuwa shambulizi la kupangwa

    (GMT+08:00) 2017-05-25 10:13:42

    Mkuu wa polisi wa Manchester Bw. Ian Hopkins amesema, polisi imethibitisha mlipuko uliotokea katika uwanja wa Manchester ni shambulizi lililopangwa, na msako dhidi ya walioshirikiana na mshambuliaji unaendelea.

    Mshambuliaji wa mlipuko huo ametambuliwa kuwa ni Salman Abedi mzaliwa wa Manchester kutoka familia ya wahamiaji wa Libya. Polisi wa Manchester wametangaza kuwakamata watuhumiwa saba wa mlipuko huo akiwemo kaka wa Salman Abedi.

    Habari pia zinasema idara ya usalama ya Libya imewakamata mdogo wa mshambuliaji wa mlipuko wa Manchester Hashem Abedi, aliyepanga kufanya shambulizi huko Tripoli. Hashem amethibitisha kuwa yeye na kaka yake ni wafuasi wa kundi la IS. Baba yao pia amekamatwa kwa kuwa na uhusiano na kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako