• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa ripoti ya utafiti wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-05-25 16:48:04

    Wizara ya biashara ya China imetoa ripoti ya utafiti wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, ikionesha kwamba pande zote mbili zimepata maslahi makubwa yenye uwiano kutokana na uhusiano huo.

    Ripoti hiyo imefafanua kuwa maslahi ya China na Marekani yameunganishwa pamoja kwenye uhusiano huo, na nchi hizo zinatakiwa kushughulikia tofauti kati yao kwa njia mwafaka, kupanua ushirikiano halisi, na kuwanufaisha wananchi wa pande mbili.

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Sun Jiwen amesema China ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea na Marekani ikiwa ni nchi kubwa zaidi iliyoendelea, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo si kama tu unaathiri maendeleo ya pande mbili, bali pia unaathiri mwelekeo wa uchumi wa dunia. China inapenda kushirikiana na Marekani na kutimiza maendeleo yenye uwiano ya biashara na uwekezaji kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako