Umoja wa ulaya umeipa Tanzania dola milioni 200 za kuendeleza sekta yake ya kawi.
Miradi ya usambazaji wa umeme chini ya ufadhili huo inatarajiwa kuwanufaisha wakaazi wa maeneo ya Kagera, Geita na Kigoma.
Kiongozi wa EU nchini Tanzania Roeland Van de Geer, amesema kuwepo na kawi ya kutegemewa kutasaidia kupunguza umaskini na pia kuahidi msaada zaidi kwa maeneo mengine ya Tanzania.
Matumizi ya kawi kwa mwaka kwa kila mtu nchini Tanzania ni kilowati 100 lakini usalishaji unasalia wa chini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |