• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatangaza kikosi cha raga kitakachochuana na Ujerumani

    (GMT+08:00) 2017-05-26 09:17:30

    Wenyeji Kenya wametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachovaana na Ujerumani katika mechi ya kimataifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande itakayochezwa kesho jijini Nairobi.

    Katika kikosi cha wachezaji 30 kilichokuwa nchini Afrika Kusini kati ya Mei 12 na Mei 22, ni wachezaji 20 waliosalia. Wilson K'Opondo na Darwin Mukidza ambao walikosa safari ya Cape Town kwa sababu za kikazi na majukumu ya timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande, mtawalia, wamo kikosini.

    George Asin, Ronnie Mwenesi, Isaac Adimo, Elkeans Musonye, Peter Kilonzo, Brad Owako, Alex Olaba, James Kubau na Emmanuel Mavala walikuwa Afrika Kusini, lakini hawajapata namba. Mchezaji wa kimataifa Joshua Chisanga anayesakata raga yake ya malipo katika klabu ya Newcastle Falcons nchini Uingereza pia hakuweza kuingia kikosini.

    Nao wachezaji Philip Ikambili, Oscar Simiyu, George Nyambua, Bramwel Mayaka na Leo Seje, ambao walikuwa nchini Afrika Kusini, wamo mbioni kuchezea Kenya kwa mara ya kwanza kabisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako