• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanne wafariki baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-05-26 09:29:10

    Wachimbaji madini wanne wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka jana kwenye eneo la Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania. Kamanda wa polisi kanda ya Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha ajali hiyo na kusema ilitokea jana asubuhi kwenye eneo lililoko kando ya magharibi ya ziwa Victoria, wakati wachimbaji 7 walipokuwa wakifanya kazi kwenye mgodi huo. Ofisa huyo amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako