• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu wa wizara ya mambo ya ndani wa Libya alaani shambulizi la Machester

    (GMT+08:00) 2017-05-26 18:15:52

    Katibu wa wizara ya mambo ya ndani wa Libya Abdossalam Ashour amelaani shambulizi la bomu lililotokea Manchester na vitendo vyote vya kigaidi vinavyowalenga raia.

    Ashour amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na Uingereza kutafuta mitandao ya kigaidi iliyohusika katika shambulizi hilo. Amesema waziri mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj amemuhakikishia mwenzake wa Uingereza Bi. Theresa May, na kusisitiza kuongeza mawasiliano na uratibu kati ya nchi hizo mbili katika kupambana na ugaidi.

    Amesema Libya haiwezi kukaa kimya katika mapambano dhidi ya ugaidi, na itasimama thabiti kuunga mkono juhudi za kutokomeza ugaidi, katika ngazi ya taifa au ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako