• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Rwanda Air yanunua ndege mpya

    (GMT+08:00) 2017-05-29 20:02:33

    Kampuni ya ndege ya Rwanda Air imenunua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 itakayotumika kusafirisha abiria katika sehemu za magharibi mwa Afrika.

    Kwa mujibu wa maafisa wakuu wa kampuni hiyo,ndege hiyo inafikisha idadi ya 12 ya ndege zote za jumla za kampuni hiyo.

    Chance Ndagano mkurugenzi mkuu wa Rwanda Air ameaihidi kwamba wana lenga kufika viwango sawa na huduma za kampuni kuu za ndege Afrika .

    Aidha huduma za Rwanda Air zimeanza kuimarika nchini humo kutokana na ukuwaji wa kasi wa uchumi unaovutia wawekezaji mara kwa mara kutoka nchi za ulaya.

    Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 154.Itasafirisha abiria katika nchi za Mali,Guibea ,Senegal .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako