• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya na Angola yafutiliwa mbali

    (GMT+08:00) 2017-05-30 08:46:11
    Timu ya Taifa ya soka ya Kenyas Harambee Stars, imeanza mazoezi yake licha ya mechi yao ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Angola iliyopangwa kuchezwa June 4, kufutiliwa mbali.

    Mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini Kenya, Nick Mwendwa, amethibitisha kuwa timu ya taifa ya Angola haitaweza kucheza mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Kenya, kwa sababu itakuwa nchini Ureno kwa mazoezi.

    Hata hivyo, Harambee Stars itaweka kambi ya mazoezi kujiandaa kushiriki katika mashindano ya ukumbusho wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, yatakayoanza Juni mosi hadi 4 jijini Kigali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako