• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: Kamworor aridhika na nafasi ya 3 mita 5,000 Amerika

    (GMT+08:00) 2017-05-30 08:46:56
    Mwanariadha Geoffrey Kamworor hakuwa na lake katika mbio za mita 5,000 kwenye duru ya 3 ya riadha za Diamond League mjini Eugene nchini Marekani, Jumamosi usiku

    Muingereza Mohamed Farah alitwaa ubingwa kwa dakika 13:00.70 nao Yomif Kejelcha kutoka Ethiopia (13:01.21) na bingwa mara mbili wa nusu-marathon duniani Kamworor (13:01.25) waliridhika katika nafasi za pili na tatu.

    Ronald Kwemoi naye alitimka kasi ya juu mwaka huu wa 2017 aliposhinda mbio za maili moja kwa dakika 3:49.04. Aliongoza Wakenya Elijah Manangoi (3:49.08), Timothy Cheruiyot (3:49.64) na Vincent Kibet (3:51.17) kumaliza katika nafasi nne za kwanza.

    Bethwell Birgen aliridhika katika nafasi ya tisa (3:53.50), Silas Kiplagat wa 12 (3:57.59) naye bingwa wa Olimpiki na dunia mita 1,500 Asbel Kiprop akaambulia nafasi ya 13 (3:58.24). Wakenya Elijah Kiptoo na Andrew Rotich hawakumaliza mashindano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako