• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Japan zafanya mazungumzo ya nne ya kisiasa ya ngazi ya juu

    (GMT+08:00) 2017-05-30 10:07:36

    Mjumbe wa taifa wa China Bw Yang Jiechi na mshauri wa usalama wa taifa wa Japan Bw Shotaro Yachi wameendesha kwa pamoja mazungumzo ya nne ya kisiasa ya ngazi ya juu kati ya nchi zao mjini Tokyo.

    Bw. Yang amesema hivi sasa, uhusiano kati ya China na Japan unakabiliwa na changamoto mpya, zinazotaka pande hizo mbili kufuata kanuni ya kushirikiana, kutotishiana na kujiendeleza kwa pamoja, kuheshimu historia, kulinda msingi wa kisiasa na kudhibiti tofauti zilizopo ili kuboresha uhusiano huo.

    Bw. Yang pia amesisitiza kuwa China inaitarajia Japan ishirikiane na China katika kujenga uaminifu wa kisiasa kati yao, na kutoa mchango katika utatuzi wa masuala ya Taiwan na Bahari ya Kusini ya China. Pia amesema China inaikaribisha Japan kujiunga kwenye pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ili kuongeza mawasiliano na maelewano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako