• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani yasema hakuna mvutano kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-05-31 09:32:31

    Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw Sigmar Gabriel amesema hakuna mvutano kati ya Ujerumani na Marekani kufuatia kauli zilizotolewa na viongozi wa nchi hizo mbili juu ya uhusiano kati yao.

    Bw Gabriel amesema ni kweli kuna hali ngumu kwenye uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani, lakini anaamini kuwa baadaye pande mbili zitarudi kwenye uhusiano wa kawaida.

    Kufuatia mkutano usio na mafanikio wa kundi la nchi 7, ambao Bw Trump alipinga makubaliano ya Paris kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupinga biashara huria, Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel alisema Ulaya inatakiwa kuangalia hatma yake yenyewe.

    Bw Trump amejibu kwa kusema Marekani ina urali mbaya wa biashara na Ujerumani, na haitoi mchango kwa NATO kama inavyotakiwa, hali ambayo ni mbaya kwa Marekani na inatakiwa kubadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako