• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Treni ya kwanza ya mizigo ya SGR yazinduliwa

    (GMT+08:00) 2017-05-31 09:32:58

    Hatimaye treni ya kwanza ya mizigo inayopita kwenye reli ya Kisasa SGR, kati ya Mombasa na Nairobi imezinduliwa rasmi.

    Uzinduzi wa reli hiyo uliongozwa na rais Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake Bw William Ruto, na kuhudhuriwa na maofisa wa serikali ya China na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji. Rais Kenyatta amewapongeza wote waliofanikisha mradi huo, ambao amesema utapunguza gharama za usafiri na kuvutia wawekezaji.

    Ujenzi wa mradi huu wa reli ya kisasa umefanyika kwa muda wa miaka miwili, na kupitia changamoto nyingi, ikiwemo upatikanaji wa ardhi na kuhakikisha makazi ya wanyama hayaharibiwi.

    Mwenyekiti wa bodi ya reli nchini Kenya Bw James Kianga amesema mafanikio ya ujenzi wa reli hiyo yametokana na ushirikiano mkubwa uliooneshwa kati ya wadau.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako