• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Martin Keown amshauri Wenger kuwauza Sanchez na Ozil

    (GMT+08:00) 2017-06-01 09:31:13

    Mlinzi wa zamani wa klabu ya Arsenal Martin Keown amesema kuwa meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger anapaswa kuwauza nyota wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil baada ya kuongeza muda wa kusalia kinoa miamba hiyo ya London.

    Mfaransa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na amesema kuwa timu yake inaweza kupigana na kutwaa ubingwa msimu ujao.

    Viungo Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwa pamoja wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa mwaka huu.

    Kewon anasema kuliko kupata hasara ya kuwaruhusu kuondoka bure ni vyema akafanya maamuzi magumu ya kuwauza nyota hao na kutengeneza faida itakayoweza kuleta wachezaji wapya na wenye morali kubwa zaidi.

    Sanchez amefunga magoli 24 na kuchangia kupatikana kwa mengine 10 huku Ozil akifunga manane na kuchangia tisa lakini hiyo haikutosha kuifanya timu hiyo kukosa michuano ya mabingwa wa Ulaya msimu ujao jambo ambalo linatia ukakasi kwa Sanchez na Ozil kuongeza mikataba yao.

    Sanchez amepewa ofa ya paundi 300,000 kwa wiki lakini bado hajasaini mkataba huo, huku Ozil akikataa paundi 250,000 kwa wiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako