• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda kujenga reli yake wakati Kenya ikihakikisha kujenga hadi makani

    (GMT+08:00) 2017-06-01 19:05:14

    Waziri wa fedha wa Uganda, Matia Kasaija amesema serikali ya nchi hiyo inasubiri Kenya kuamua iwapo itajenga sehemu yake ya reli ya kisasa hadi kwenye eneo la mpakani ili nayo Uganda ianze ujenzi upande wake.

    Benki ya Exim ya China itafadhili Uganda kujenga reli lakini ni baada ya kuhakikisha kwamba Kenya inn uwezo wa kujenga sehemu yake.

    Kenya imetangaza ingependa kujenga reli hadi kwenye mpaka wake na Uganda lakini inapanga kuanza ikiwa kwenye nafasi ya kukopa fedha zaidi.

    Benki hiyo ya Exim itatoa asilimia 85 ya ufadhili wa reli hiyo ya Uganda ambayo itajengwa kwa dola bilioni 2.3.

    Reli hiyo ya kilomita 273 itaunganisha eneo la mpakani la Malaba na mji mkuu Kampala.

    Tayari awamu ya kwanza ya reli ya kisasa ya Kenya imekamilika na imefunguliwa kusafirisha shehena na abiria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako