• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rufaa ya Atletico Madrid yapigwa na chini na CAS

    (GMT+08:00) 2017-06-02 11:21:34

    Klabu ya Atletico Madrid imeshindwa katika rufani yao waliyokata katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu ya kuzuiwa kusajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.

    Hatua hiyo sasa inamaanisha kuwa klabu hiyo haitaruhusiwa kusajili mpaka utakapofika usajili wa dirisha doko Januari 2018.

    Atletico walifungiwa kusajili kwa vipindi viwili vya usajili kwa kosa la kukiuka sheria ya usajili wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya miaka 18.

    Baada ya kushindwa rufani yao FIFA, Atletico walitumikia adhabu ya kutosajili katika dirisha la Januari mwaka huu kabla ya kuamua kukata rufaa CAS. Kutokana na matokeo ya rufani yao Atletico sasa watakuwa

    wameshindwa kufanya usajili wowote kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako