• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (27 Mei-2 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-02 20:48:37

    Serikali ya Libya yatwaa uwanja wa ndege wa Tripoli

    Walinzi wa rais wa Libya wametangaza kuwa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imetwaa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli.

    Kamanda wa walinzi wa rais Bw. Najmi Nakoo amesema serikali imedhibiti uwanja huo, na jeshi la serikali pia limefanikiwa kutwaa baadhi ya kambi za jeshi na maeneo kusini mwa Tripoli yaliyodhibitiwa na makundi ya waasi awali.

    Tarehe 27 Mei, jeshi la serikali kwa kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa lilipambana na wapiganaji wanaotii serikali ya Khalifa al-Ghawil iliyopinduliwa kusini mwa Tripoli, na mapambano hayo yamesababisha vifo vya watu 55 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako