• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya Sportpesa Super Cup kuanza leo

    (GMT+08:00) 2017-06-05 08:18:16

    Michuano ya Sportpesa Super Cup inatarajiwa kuanza leo jijini Dar es salaam Tanzania michezo itakayochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

    Michuno hiyo itazikutanisha timu 4 kutoka Tanzania na timu 4 kutoka Kenya katika kuwania kitita cha Dola za kimarekani elfu thelathini (US $ 30,000) na mshindi wa fainali hizo atapata nafasi ya kuvaana na timu ya Everton kutoka Ligi kuu ya England mwezi Julai tarehe 13.

    Mechi ya kwanza itakuwa baina ya AFC Leopards ya Kenya kuchuana na Singida United huku mabingwa wa Vodacom Premier League Yanga SC wakichuana na mabingwa wa SportPesa Premier League Tusker FC ya Kenya siku ya tarehe 6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako