• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni Real Madrid tena, wanyakua ubingwa kwa kuibamiza Juventus 4-1

    (GMT+08:00) 2017-06-05 08:19:13

    Real Madrid ya Hispania imefanikiwa kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Juventus ya Italia usiku wa jumamosi kwenye uwanja wa Millennium mjini Cardiff, Wales.

    Mwanasoka bora wa dunia, Mreno Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili, moja kila kipindi, huku mabao mengine yakifungwa na Casemiro na Marco Asensio na la Juve limefungwa na Mario Mandzukic kukamilisha msimu wa Ligi ya Mabingwa 2017.

    Hilo linakuwa taji la 12 la michuano hiyo kwa Real Madrid tangu inaitwa Klabu Bingwa Ulaya, baada ya awali kulitwaa katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014 na 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako