• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwanini hatuwezi kuangamiza kabisa panya

    (GMT+08:00) 2017-06-05 18:14:05

    Panya wanaiba chakula na kuambukiza maradhi. Binadamu wamefanya majaribio katika maelfu ya miaka iliyopita, lakini bado kuna panya wengi sana duniani. Kwanini hatuwezi kuwaangamiza kabisa wanyama hawa?

    Bila shaka panya ni mmoja kati ya wanyama wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuishi duniani. Panya wana mayopia na upofu wa rangi, lakini wana uwezo mkubwa wa kusikia, kuhisi harufu na ladha, wanaweza kusikia sauti aina ya ultrasonic isiyosikika kwa sikio la binadamu, kutofautisha chakula kibaya, hata anaweza kuhisi chakula chenye ladha ndogo sana isiyo kawaida, tena wanajificha kwenye mashimo, wana tahadhari kubwa, hivyo si rahisi kuwakamata. Jambo muhimu zaidi ni kwamba panya wana uwezo mkubwa sana wa kuzaliana. Kwa mfano, muda wa kubeba mimba wa panya aina ya Apodemus agrarius ni siku 21 tu, na siku ya pili baada ya kuzaa watoto, panya jike anaweza kupata mimba tena. Panya wadogo waliozaliwa katika majira ya mchipuko wanakomaa na kuanza kuzaa katika majira ya mpukutiko. Hivyo binadamu wakilegeza kazi ya kuwaangamiza, idadi yao itafufuka mara moja.

    Jambo zuri ni kwamba ingawa ni vigumu kwa binadamu kuwaangamiza panya, lakini kwauondoa panya kwenye nyumbani bado ni kazi rahisi. Tukifunika chakula ndani ya vyombo mbalimbali na kusafisha nyumba zetu, si kama tu panya wa nje hawatakuja, bali pia panya wa nyumbani watahama kutokana na ukosefu wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako