• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan:China yatoa msaada wa dawa na matibabu ya Malaria

    (GMT+08:00) 2017-06-06 18:42:27
    China imetoa zaidi ya visanduku nusu millioni kwa nchi ya Sudan Kusini ili kuwasaidia kukabiliana na janga la Malaria.

    Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Sudan Kusini,dawa hizo ni za thamani ya dola 750,000 ikiwa ni mpango wa China wa kuisadia nchi hiyo iliyoyumba kiuchumi baada ya ghasia.

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini He Xiandong msaada huo unaashiria ushirikiano wa karibu wa kibiashara na urafiki baina ya China na Sudan Kusini.

    Waziri wa afya nchini humo Riek Gai Kok amesema nchi hiyo imefaidika pakubwa na mshikamano wa kibiashara na China tangu mwaka 2011 walipopata uhuru.

    China pia imetoa fedha na usaidizi katika sekta nzima ya afya nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako