• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Mifuko ya plastiki kupoteza samaki majini ifikiapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2017-06-06 18:42:45
    Katibu mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Antonio Guiterres ametoa onyo ya kupungua kwa samaki katika bahari ama vyanzo vingine vya maji kutokana na kutapakaa kwa mifuko ya plastiki majini.

    Katika kongamano la siku tano la mazingira ,katibu huyo amependekeza viongozi na wataalamu wa masuala ya baharini na majini kusitisha mara moja uharibifu wa mazingira ya majini akisema utaleta maangamizi makubwa kwa viumbe vya majini haswa samaki.

    Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kwamba mifuko ya plastiki inaendelea kuongezeka majini hivyo kuharibu mazingira ama eco system inayochangia afya duni kwa samaki.

    Sekta ya usimamizi wa masuala ya baharini imetakiwa sasa kuanzisha harakati za kupunguza matumizi ya plasitiki na utupaji wake baharini.

    Aidha uvuvi haramu unaotumia vifaa vinavyoshika samaki wadogo limetajwa jambo litakaloangamiza idadi ya viumbe hivyo.

    Nchini Uganda,wizara ya uvuvi imeanzisha kampeini ya kuhamasisha wavuvi dhidi ya uvuvi haramu pamoja na kuanzisha mipango ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

    Rwanda,na Tanzania zimeanzisha utekelezaji wa sheria ya kuzuia mautumizi ya mifuko ya plastiki nayo Kenya ikitarajia kuanza kutumia sheria hiyo mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako