• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgomo wa manesi watishia sekta ya afya nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-07 09:23:41

    Siku moja tu baada ya chama cha wauguzi nchini Kenya kutangaza mgomo wakenya ambao walifika kwenye hospitali mbali mbali wameelezea kusikitishwa kwao na hatua ya wauguzi hao na kuitaka serikali kufanya kila iwezalo kuhakikisha wanapata matibabu. Katika hospitali ya Samburu wagonjwa walionekana kutaabika huku wasijue watakalofanya baada ya kukosa huduma za wauguzi. John Lepere ambaye anaugua ugonjwa wa Malaria anaonekana akisaidiwa na mke wake baada ya wauguzi kugoma.

    "Tunaomba serikali iwalipe madaktari ili iweze kuokoa maisha ya watu"

    Chama cha wauguzi kimesema licha ya makubaliano kufikiwa hadi kufikia sasa wauguzi hawajapokea marupurupu yao kulingana na makubaliano. Chama hicho kinadai baraza la magavana limekuwa kikwazo kikubwa kwa utekelezaji makubaliano kuhusu matakwa yao. Hata hivyo upande wa serikali umesema wanasubiri mahakama itoe uamuzi kuhusu kesi hiyo kabla ya kuanza mchakato wa kulipa marupurupu hayo. Josphat Nanok ni mwenyekiti wa baraza la Magavana nchini Kenya. Anasema hivi sasa wanasubiri tamko la tume ya mishahara nchini Kenya kuhusu marupurupu hayo ya wauguzi.

    "Pindi tu tume ya mishahara na marupurupu itakapotoa tamko lake kuhusu swala hili, serikali kuu pamoja na serikali za kaunti zitasaini maramoja makubaliano na chama cha wauguzi . Kuhusu ni fedha ngapi zinahusishwa ni kwamba makubaliano hayo yatahitaji serikali kutoka shilingi bilioni arobaini na milioni lakini tatu na sitini na sita" anasema Nanok

    Katika hospitali nyingi wauguzi waliwaacha baadhi ya wagonjwa wakiwa katika hali ya maumivu huku wengi wao wasijue la kufanya. Katika hospitali ya Kiambu ninakutaka na Patrick Kamau ambaye ndiye Daktari mkuu katika hospitali ya kaunti hiyo.Amezitaka familia za wagonjwa hospitalini humo kuwachukua wagonjwa wao na kuwapeleka nyumbani.

    "Pia tunawashauri wale jamaa au familia wenye wagonjwa kwenye hospitali hii ya Kiambu waje wachukue wagonjwa wao"

    Mgomo huo wa manesi unakuja miezi michache tu baada ya mgomo mwingine wa madaktari uliodumu kwa zaidi ya siku 100 na kuwafanya wagonjwa wengi kutaabika huku wengine wakifariki.Hivi sasa wakenya wanasubiri kuona kama serikali itatatua mgogoro huo ndani muda mchache zaidi ili kuepuka maafa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako