• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: bei ya soda kuenda juu

    (GMT+08:00) 2017-06-07 19:32:42
    Wawekezaji katika sekta ya vinywaji vyenye kemikali ya kaboni nchini Uganda wameonya kuwa bei ya soda inaweza kwenda juu kama serikali itapitisha kodi mpya.

    Wanasema hatua hii itasababisha kupungua kwa mauzo, kazi na kushuka kwa kiwango cha mapato.

    Mwaka 2016, wawakilishi wa sekta hiyo walikutana na kamati ya bunge ya fedha, kupitisha mbele pendekezo la kupunguza ushuru wa bidhaa na kamati ilipendekeza kupunguza asilimia 3 katika mwaka wa fedha 2016/2017.

    Aprili 12, 2016,katika mkutano ulifanywa na Rais Museveni alipendekeza kupunguzwa kutoka asilimia 13-10 kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2017/2018.

    Athari za ongezeko ya kodi mpya itasababisha kushuka kwa kodi ya VAT na kusababisha kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na mauzo ya chini.

    Kampuni ya Coca-Cola katika eneo la Mbarara imesema kama kodi mpya itapitishwa basi wanaweza kufunga kiwanda hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako