• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa dola milioni tano kwa wakimbizi wa Kakuma Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:18:48

    Balozi wa China nchini Kenya Bw Liu Xianfa amesema serikali ya China itaendelea kutoa msaada wa kibinadamu ili kuboresha maisha ya wakimbizi kwenye maeneo mbalimbali nchini Kenya.

    Bwana Liu aliyasema hayo Jumatano wakati akiwasilisha msaada wa dola milioni tano uliotolewa na serikali ya China kuwasaidia wakimbizi wa kambi ya Kakuma kaskazini mwa Kenya. Fedha hizo zimetumika kuwanunulia wakimbizi mahindi na bidhaa nyinginezo za chakula.

    "Nimefurahi kuja hapa kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi wa kambi ya Kakuma. Tumetoa msaada wa dola milioni tano kwa wakimbizi wa hapa, ikiwa ni njia ya China ya kuungana na juhudi za kimataifa za kukabiliana na uhaba wa chakula. Tunapongeza Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa mataifa WFP na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kutusadia kufikisha msaada hapa na pia kwa kuungana nasi kusaidia wakimbizi."

    Kambi hiyo ina zaidi ya wakimbizi 176,800 wengi wao wakiwa ni kutoka nchini Sudan Kusini ambako wamekimbia mapigano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako