• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Novak Djokovic asema "byebye" mashindano ya wazi ya Ufaransa

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:35:43

    Novak Djokovic ameyaaga mashindano ya mchezo wa tennis yanayo endelea huko mjini Paris, Ufaransa. Mchezaji huyo ambaye alikuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo ametupwa nje kwa jumla ya Seti 7-6 (7-5) 6-3 6-0 dhidi ya mchezaji Dominic Thiem katika hatua ya robo fainali.

    Thiem ambaye ni raia wa Australia, sasa atakutana na Rafael Nadal katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa ulimwenguni baada ya kumtoa bingwa huyo mtetezi raia wa Serbia.

    Kwa upande wake, Nadal ametinga hatua ya nusu fainali baada ya kumtoa Mhispania Pablo Carreno Busta. Michezo hiyo ya hatua ya robo fainali ilichelewa kuanza kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako