• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imekuwa nchi kubwa ya pili inayowekeza nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2017-06-08 18:37:59

    Ripoti iliyotolewa jana katika Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nchi za nje duniani mwaka jana ulipungua, lakini uwekezaji wa China kwa nje umeongezeka, na kuifanya kuwa nchi kubwa ya pili inayowekeza nchi za nje.

    Ripoti hiyo kuhusu uwekezaji wa dunia mwaka 2017 inaonesha kuwa, thamani ya jumla ya uwekezaji wa moja kwa moja wa nje duniani mwaka jana ulipungua kwa asilimia 2, na kufikia dola za kimarekani trilioni 1.75. Uwekezaji wa Marekani katika nchi za nje kwa mwaka jana ulipungua kwa kiasi kidogo na kufikia dola za kimarekani bilioni 299, ambayo bado ni nchi kubwa zaidi inayowekeza nchi nyingine.

    Uwekezaji wa China katika nchi za nje kwa mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 44, na kufikia dola za kimarekani bilioni 183, na kuifanya kuwa nchi kubwa ya pili kuwekeza nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako