• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kagame azitaka Afrika na Ulaya kushirikiana zaidi

    (GMT+08:00) 2017-06-08 18:53:48
    Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema nchi za Afrika na Ulaya zinafaa kufanya kazi kwa pamoja lakini sio kutoleana vitisho.

    Kagame aliyasema hayo mjini Brussels nchini Ubelgiji wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maendeleo ya ulaya.

    Mkutano huo huandaliwa na Tume ya Ulaya ukileta pamoja jumuiya ya maendeleo duniani kubadilishana mawazo na uzoezu na pia kujadili maeneo mapya ya ushirikiano na kutafuta suluhu za changamoto za dunia.

    Kagame alitoa wito wa kuwa na ushirikiano zaidi na kuheshiniana kati ya pande zote mbili.

    Alisema maendeleo endelevu hunawiri kwenye mazingira ya siasa zuri na kuheshimu haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako