• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mkurugenzi Mpya wa Benki ya Wanawake Tanzania, anatarajiwa  kuirudisha hadhi ya benki hiyo

    (GMT+08:00) 2017-06-08 18:54:06
    Mkurugenzi Mpya wa Benki ya Wanawake Tanzania, (TWB) Japhet Justine ana kibarua kikubwa cha kuirudisha hadhi ya benki hiyo pamoja na kutatua tatizo la tozo kubwa za riba katika mikopo inayotolewa kwa wanawake.

    Bodi ya Wakurugenzi ya TWB ilimtangaza Justine kuwa mkurugenzi mpya wa benki hiyo akiwa na wasifu wa kufanya kazi katika benki za kitaifa na kimataifa.

    Aliyekuwa mkurugenzi wa benki hiyo kabla ya Justine, Margareth Chacha amestaafu.

    Miongoni mwa changamoto zinazoikabili benki hiyo ni pamoja na ile iliyotajwa na Waziri Ummy Mwalimu (anayesimamia sekta ya jinsia) kuwa benki hiyo inatoza riba kubwa ya asilimia 19 wakati inapata fedha serikalini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako